Na Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Ikiwa Ulimwengu Mzima ukikumbwa na Taharuki ya ugonjwa unaosababishwa na Virusi vya Corona ,Wizara ya Maji imefuta shughuli zote kuchukua tahadhari ya maambukizi ya virusi hivyo.
Katika taarifa iliyotolewa leo Machi 16,2020 na kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Maji ,kwa Umma imefafanua kuwa shughuli zote zilizokuwa zifanyike kuelekea siku ya maji duniani.
Hivyo,Taarifa hiyo imefafanua kuwa hafla za uzinduzi wa miradi ya maji na mikutano yote ambayo ilikuwa ifanyike katika wiki hii imefutwa huku wizara ikiomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza kwa wadau wote .
Ikumbukwe kuwa Mataifa mbalimbali yamejawa na hofu ya kuenea kwa ugonjwa wa virusi vya Corona ambapo hapa Tanzania kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amethibitisha kuwepo kwa kisa cha mtu mmoja Mtanzania mwanamke [46]ambaye aliwasili na ndege ya Rwandair akitokea nchini Ubelgiji na kushukia katika uwanja wa ndege wa KIA na alifikia katika hotel ya Mt.Meru jijini Arusha.
Social Plugin