Mkutano wa Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe uliokuwa ukifanyika jana katika kijiji cha Kikafu Chini, ulivurugwa baada ya kuibuka kikundi cha vijana zaidi ya 50 wa kike na kiume kwenye mkutano huo na kuanzisha vurugu huku wakipiga kelele wakiimba "Sema ulichofanya, tunamtaka Magufuli".
Mbowe alipanda jukwaani jana saa 11:12 jioni ambapo alizungumza hadi saa 11:47 jioni ndipo kundi la vijana lilipoibuka na kuanza kupiga kelele, jambo lililomfanya mbunge huyo kunyamaza.
Hata hivyo kabla ya kunyamaza, Mbowe alisema polisi hili ndilo kundi ambalo tuliwaambia na baada ya kauli hiyo alinyamaza akiangalia vurugu hizo.
Vijana hao wanaodaiwa kutoka maeneo mbalimbali walianza kupiga kelele wakisema "sema ulichofanya, tunataka Magufuli” hali ambayo iliwafanya polisi kuingilia kati kuanza kutuliza vurugu hizo.
Baada vurugu kuendelea, polisi ambao walikuwa na gari moja waliongeza nguvu kwa kuja polisi waliokuwa wamevalia sare na kudhibiti kikundi hicho kusogelea jukwaa alilokuwa amesimama Mbowe.
Alivyonyamaza zaidi ya dakika 20 akiwatizama bila kuongea chochote polisi nao walisimama ili wasiende kwenye jukwaa alilokuwa Mbowe.Baadaye waliondoka
Social Plugin