Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe akiwa ameambatana na Kaimu Katibu Mkuu Dorothy Semu na Katibu Mwenezi Ado Shaibu wamekabidhi kiasi cha Tsh. Milioni 2 ikiwa ni kusaidia kulipa faini zinazowakabili viongozi wa CHADEMA baada ya kuhukumiwa jana katika kesi iliyowakabili Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam.
Fedha hizo zimepokelewa leo March 11, 2020 na Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar, Said Issa Mohammed katika Ofisi za Makao Makuu ya CHADEMA, Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Itikadi, uhusiano na mambo ya nje wa Chadema, John Mrema amesema mbali ya kutoa fedha hizo, Zitto ameahidi kuhamasisha wanachama wa ACT-Wazalendo kuchangia Chadema.
Tangu jana Zitto aliandika kwenye ukursa wake wa Twitter akisisitiza kushirikiana na Chadema kuhamasisha wananchi kuchangia faini hiyo.
Social Plugin