Idadi ya maambukizi ya virusi vya Corona nchini Afrika Kusini imefika watu 5,350 baada ya visa vipya 354 kuthibitishwa, huku idadi vifo ikifikia watu 103.
Taarifa kutoka wizara ya afya imesema visa vipya 354 ni vya juu kuwahi kuripotiwa nchini humo chini ya kipindi cha saa 24.
Takriban wiki sita zimepita tangu kisa cha kwanza cha Covid 19 kuripotiwa nchini Afrika Kusini, na idadi ya maambukizi imekuwa ikiongezeka .
Hivi karibuniAfrika Kusini ilichukuwa mikakati mipya kupambana dhidi ya Corona katika magereza mbalimbali nchini humo, baada ya wafungwa 59 na wafanyakazi wa gereza 29 kuthibitishwa kuambukizwa katika kipindi cha majuma mawili.
Social Plugin