Breaking : GARI YAUA WATU WANNE BAADA YA KUTUMBUKIA BWAWANI BARABARA YA OLD SHINYANGA

Gari yenye namba za usajili T.785 DBM Toyota IST ikiopolewa ndani ya bwawa la maji lililopo pembezoni mwa barabara ya vumbi ya Old Shinyanga  iliyoua watu wanne leo Aprili 4,2020.


Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog 
Watu wanne wamefariki dunia baada ya gari waliyokuwa wanasafiria kugonga gema kisha kutumbukia katika bwawa la maji lililopo pembezoni mwa barabara ya vumbi ya kutoka Old Shinyanga kuelekea Bubiki hadi Mwanza kwenye kijiji cha Bubiki B kata ya Bubiki wilaya ya Kishapu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba amesema ajali hiyo ya gari kuacha njia na kugonga gema na kutumbukia katika bwawa la maji na kusababisha vifo imetokea leo Jumamosi Aprili 4,2020 majira ya saa saa tatu na dakika 20 asubuhi katika eneo la kitongoji cha Mwajinaganya kijiji cha Bubiki B, kata ya Bubiki, tarafa ya Mondo, wilaya ya Kishapu. 

“Ajali hii imetokea katika barabara ya vumbi ya kutoka Old Shinyanga kuelekea Bubiki hadi Mwanza ambapo ,gari yenye namba za usajili T.785 DBM Toyota IST iliyokuwa ikiendeshwa na dereva aitwaye Gration Mlikozi, miaka haifahamiki ikitokea Old Shinyanga kuelekea barabara kuu ya kwenda Mwanza ilipoteza uelekeo na kugonga gema na kutumbukia katika bwawa la maji lililochimbwa kwa ajili ya kuchukulia udongo wa matengenezo ya barabara na kusababisha vifo kwa watu wanne”,ameeleza Kamanda Magiligimba. 

Amewataja waliofariki dunia katika ajali hiyo kuwa ni dereva wa gari hilo Gration Mlikozi pamoja na abiria watatu ambao ni Singu Isack Lazaro (57), Chrispin Ikate, miaka haijulikani, mwanaume, na Abdallah Mussa, mwanaume, miaka haifahamiki. 

“Chanzo cha ajali ni mwendokasi wa gari husika katika barabara ya vumbi kulikopelekea dereva gari kumshinda na kwenda kugonga gema na kutumbukia katika bwawa la maji na kusababisha vifo”,amesema. 

“Gari husika limeshatolewa katika maji na lipo katika kituo cha polisi Maganzo. Miili ya marehemu imehifadhiwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga. Natoa wito kwa madereva wote kutii sheria za usalama barabara na kuacha kuendesha vyombo vya moto kwa mwendo kasi”,amesema Kamanda Magiligimba.

Gari yenye namba za usajili T.785 DBM Toyota IST ikiopolewa ndani ya bwawa la maji lililopo pembezoni mwa barabara ya vumbi ya Old Shinyanga  iliyoua watu wanne leo Aprili 4,2020  katika eneo la kitongoji cha Mwajinaganya kijiji cha Bubiki B, kata ya Bubiki, tarafa ya Mondo, wilaya ya Kishapu barabara ya Old Shinyanga kuelekea Bubiki - Mwanza . Picha na Malunde 1 blog

Sehemu ya bwawa hilo.

Gari yenye namba za usajili T.785 DBM Toyota IST ikitolewa bwawani na Trekta baada ya kugonga gema na kutumbukia katika bwawa hilo na kuua watu wanne.
Kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba  akiwa katika eneo la kitongoji cha Mwajinaganya kijiji cha Bubiki B, kata ya Bubiki, tarafa ya Mondo, wilaya ya Kishapu barabara ya Old Shinyanga kuelekea Bubiki - Mwanza ambapo gari yenye namba za usajili T.785 DBM Toyota IST imegonga gema na kutumbukia bwawani na kusababisha vifo vya watu wanne. Picha na Malunde 1 blog
Gari yenye namba za usajili T.785 DBM Toyota IST iliyokuwa ikiendeshwa na dereva aitwaye Gration Mlikozi iliyopoteza uelekeo na kugonga gema na kutumbukia katika bwawa la maji lililopo pembezoni mwa barabara ya vumbi ya Old Shinyanga na kuua watu wanne.Picha na Malunde 1 blog
Gari yenye namba za usajili T.785 DBM Toyota IST iliyokuwa ikiendeshwa na dereva aitwaye Gration Mlikozi iliyopoteza uelekeo na kugonga gema na kutumbukia katika bwawa la maji lililopo pembezoni mwa barabara ya vumbi ya Old Shinyanga na kuua watu wanne.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post