Jeneza lenye mwili wa Askofu na mbunge wa Viti maalum CCM Mkoa wa Morogoro mama Getrude Rwakatare likiwa tayari kuingizwa kaburini huku likiwa limefunikwa bendera ya bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa mazishi yaliyofanyika kwenye viunga vya kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni B jijini Dar es salaam leo.
--------
Mwili wa Askofu/Mchungaji wa Kanisa la Mlima wa Moto, Mikocheni B, Assemblies of God, Dkt Getrude Rwakatare ambaye ni mbunge wa Viti Maalum CCM Mkoa wa Morogoro umepumzishwa katika nyumba yake ya milele, katika viunga vya kanisa hilo, jijini Dar es Salaam.
Mazishi hayo yamefanyika leo Alhamis Aprili 23, 2020, majira ya saa 7:00 mchana na kuhudhuriwa na watu wachache wakiwemo wakiwemo wawakilishi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na baadhi ya ndugu kuepuka msongamano kutokana na kusambaa kwa maambukizi ya Virusi vya Corona.
Mama Rwakatare alifariki Dunia Aprili 20, 2020, katika hospitali ya Rabininsia, alikokuwa akipatiwa matibabu, ambapo kwa mujibu wa mwanaye Mutta Rwakatare, alisema kuwa Mama yao alikuwa akisumbuliwa na tatizo la moyo na presha.
Baadhi ya Waombolezaji wakiwa katika mazishi ya aliyekuwa Askofu na mbunge wa Viti Maalum CCM Mkoa wa Morogoro Mama Getrude Rwakatare yaliyofanyika kwenye kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni B jijini Dar es Salaam leo.
Social Plugin