Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ATIWA MBARONI KWA KUMUUA MKEWE BAADA YA KUMFUMANIA NA MWANAUME MWINGINE NDANI YA NYUMBA YAO

Tukio la kwanza
Tarehe 10.04.20202 majira ya 04:00hrs alfajiri, huko kijiji cha Nyamanga, kata ya Ukara, wilayani Ukerewe, Pastory Majura, miaka 52, msukuma, Mkazi wa kijiji cha Nyamanga – Ukerewe, anatuhumiwa na kosa la mauaji baada ya kumuua

Mkewe aitwaye Anusiata James, miaka 52, mzinza, Mkazi wa kijiji cha Nyamanga, kwa kumpiga Kichwani na kitu kizito baada ya kumfumania mke Wake nyumbani kwake akiwa na mwanaume Mwingine ambaye alikimbia baada ya mtuhumiwa Kumkuta nyumbani kwake.

Mume wa marehemu ambaye kwa sasa ni Mtuhumiwa mara baada ya kumshambulia na Kumuua mkewe aliamua kujichoma tumboni na kitu Chenye ncha kali ambapo alipata maumivu makali Na kukimbizwa hospitali ya wilaya ya ukerewe kwa matibabu. Upelelezi wa shauri hili unakamilishwa na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo.

Mwili wa marehemu tayari umefanyiwa uchunguzi Na daktari na kukabidhiwa kwa ndugu wa Marehemu kwa ajili ya mazishi.

Kuelekea sikukuu ya pasaka.
Jeshi la polisi mkoa wa mwanza kwa kushirikiana Na vyombo vingine vya usalama limejipanga vizuri Kuhakikisha sikukuu ya pasaka inasheherekewa Kwa amani na utulivu.

Linasisitiza wananchi kujiepusha na misongamano isiyo ya lazima kwani adui wetu mkubwa kwa sasa ni virusi vya corona (covid 19), lakini jeshi linatoa onyo juu ya watu wanaopanga kujaribu hata kuwa kwenye nafasi ya kutaka kutekeleza uhalifu kwamba atakaejaribu jeshi halitasita kumkamata kabla na hatua za kisheria zitachukuliwa.

Jeshi la polisi mkoa wa mwanza linaendelea Kuwashukuru wananchi wote wanaoendelea Kutoa taarifa za wahalifu na uhalifu ili Wakamatwe kabla ya matukio na linaendelea Kujielekeza katika mfumo wa kimaadili wa Kutotoa siri ya watoa taarifa. Jeshi linawatakia Sikukuu njema ya pasaka.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com