
Idadi ya wagonjwa wa Corona Tanzania imeongezeka nakufikia 147 baada ya wagonjwa wapya 53 kukutwa na virusi hivyo.
Akiongea na vyombo vya habari leo Ijumaa April 17,2020, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema wagonjwa wote hao ni watanzania ambapo 38 ni kutoka Dar es Salaam,10 Zanzibar,Kilimanjaro 1,Mwanza 1,Pwani 1,Lindi 1,na Kagera 1
Amesema wagonjwa hao wapya wamebainika baada ya sampuli kupimwa katika Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii jana Aprili 16 na leo Aprili 17.
Amesema hadi sasa kuna jumla ya watu 147 waliopata maambukizi ya virusi vya Corona (COVID-19) nchini, kati yao waliopona ni 11 na vifo 5 vimethibitishwa tangu kuanza kuripotiwa kwa ugonjwa huu nchini Machi 16, mwaka huu.
Amesema Wagonjwa wote waliobaki (131) hali zao ni nzuri isipokuwa wanne ambao wanapatiwa matibabu ya wagonjwa mahututi kutokana na kuwa wanasumbuliwa na matatizo mengine ya kiafya.
Msikilize hapo chini
Social Plugin