Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema wagonjwa wengine 2 wa Corona hapa nchini wamepona na kufanya idadi ya waliopona kufika 5 huku kifo kikiwa ni kimoja.
Amesema kati ya wagonjwa hao, Dar es Salaam - 1 na Arusha - 1. Hivyo sasa Mkoa wa Arusha hauna mtu mwenye maambukizi ya COVID19.
Waziri Ummy amewataka Watanzania waendelee kuzingatia maelekezo ya Wataalam wa Afya ikiwemo kuepuka mikusanyiko na misongamano isiyo ya lazima
Social Plugin