Virusi vya corona Covid-19 vimefanya uharibifu katika kila sekta ya maisha yetu duniani kuanzia China, Marekani bara Asia hadi Afrika.
Huku tukikabiliana na changamoto hii mpya, ni muhimu kutathmini na kutumia kila kifaa tulichonacho ili kupumguza maambukizi, vifo na mateso ya mlipuko huu.
Kutokaribiana, kuosha mikono na kujitenga kunaweza kupunguza maambukizi. Lakini je chakula na lishe bora kinaweza kuwa na jukumu gani katika mlipuko huu?
Tunaamini kwamba kuna njia tatu muhimu za utaratibu maalumu wa chakula ambazo zinaweza kukabiliana na tatizo hilo la kiafya.
Virutubishi
Kwanza, ulaji wa kiwango cha juu cha virutubishi fulani huimarisha mfumo wa kinga, huku ulaji wa kiwango cha chini ukidhoofisha kinga na kuvutia maradhi ya maambukizi.
Kinga imara mwilini inaweza kusaidia kukabiliana na virusi , na pia inaweza kuwasaidia baadhi ya wagonjwa kupona kwa haraka.
Virutubisho vinavyoweza kuimarisha kinga ya mwilini ni kama vile madini ya zinc, Selenium, iron na vitamin A,C,D,E , B-6 mbali na vyakula kama vile kama goji berry, broccoli, chai ya kijani, na manjano.
Mboga na matunda kama vile maembe, mananasi na tufaa ni muhimu katika kuimarisha kinga dhidi ya magonjwa ya milipuko.
Baadhi ya madaktari wanasema kwamba matunda kama vile machungwa yana vitamin C nyingi ambayo ina uwezo wa kukabiliana na magonjwa.
Baadhi ya virutubishi hivi vinasaidia kuzuia uvimbe kupitia kiasi na uharibifu wa tishu unaosababishwa na virusi hivyo ambao unaweza kusababisha majeraha ya mapafu na hata kifo.
Ni mapema mno kujua ni mchanganyiko gani wa virutubisho ndio bora kukabiliana na covid-19.
Lakini tunajua kwamba baadhi ya virutubisho hivyo vimeonesha kukabiliana na homa ya kawaida na magonjwa mengine ya mapafu.
Huku mikahawa mingi ikiwa imefungwa, chukua fursa hii kula vyakula vyenye afya nyumbani kama vile machungwa, matunda, broccoli, mboga ya mchicha, uyoga, pilipili nyekundu, viazi vitamu, samaki, maharagwe, siagi, manjano na chai.
Vyakula hivi vinaweza kuwa muhimu kwa watu wazima ambao hula kiwango kidogo cha vyakula hivi na ambao wako hatarini zaidi kuambukizwa maradhi ya Covid-19.
Lishe duni
Pili uzoefu kutokana na milipuko mengine ya magonjwa ya maambukizi unaonesha wazi kwamba watu wanaokula lishe duni wako hatarini zaidi kuambukizwa virusi hivi.
Pia wanaweza kuwa wagonjwa kwa kipindi kirefu na hata kupoteza maisha yao. Katika mlipuko huu kuwalisha watu waliopo katika hatari kupata mambukizi haya ni muhimu zaidi.
Na hatimaye mbali na umri mkubwa, hatari ya maambukizi ya Covid-19 na vifo iko juu miongoni watu wanaougua magonjwa mengine kama vile yale ya moyo, na sukari.
Hali hii hudhoofisha uwezo wa moyo kukabiliana na shinikizo la mawazo huku kisukari kikidhoofisha mfumo wa kinga.
CHANZO - BBC