Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

CHIFU MAARUFU KIJIJINI AZIKWA NDANI YA GARI LAKE ANALOLIPENDA

Mazishi ya Tshekede Pitso

Chifu Tshekede Pitso wa kijiji kimoja Jozanashoek Sterkspruit, Eastern Cape nchini Afrika Kusini amewaacha wengi vinywa wazi baada kuzikwa ndani ya gari lake alilopenda sana enzi za uhai wake la Mercedes Benz.

Inaelezwa  kuwa chifu huyo alikuwa ameagiza familia yake kuheshimu matakwa yake kwa kumzika ndani ya gari hilo lenye gharama ghali.

Chifu Pitso, ambaye alifariki akiwa na miaka 72, alivutwa na trela hadi katika kaburi lake akiwa amevalia suti nyeupe huku mikono yake yote ikiwa imeshikilia 'steering' kana kwamba alikuwa hai. 

Kulingana na binti wa chifu huyo, Sefora Letswaka, marehemu alipenda sana gari hilo la Mercedes Benz E500 licha ya kuwa lilikuwa limeharibika.

 "Kwa wakati mmoja baba yangu alikuwa mwanabiashara tajiri ambaye alikuwa na kundi la magari ya Mercedes. Miaka miwili iliyopita, alijinunulia Mercedes Benz iliyokuwa imetumika. 

Haikuchukua muda kabla ya gari hilo kuharibika, lakini muda wake mwingi alikuwa akiketi ndani ya gari hilo. Hakuwa analiendesha lakini hapo ndipo alikuwa anapata furaha na kusema wakati utakapofika angependa kuzikwa ndani yake. Tulimsikiza na kutimiza matakwa yake na ninatumai amefurahi," alidokezea Sefora.

 Baba huyo wa watoto sita alifanyiwa mazishi rasmi ya dini ya kikristu katika boma la familia hiyo Afrika Kusini. 

Mazishi ya mwanasiasa huyo wa Chama cha United Democratic Movement iliwashuhudia watu wengi wakihudhuria ambao waliamua kuvunja sheria ya kutoka nje kutokana na Janga la Corona. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com