Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

CORONA YASAMBAA KATIKA NCHI 50 AFRIKA


Kituo cha udhibiti na kuzuia magonjwa vya Umoja wa Afrika kimesema kuwa watu 172 wamepoteza maisha baada ya kuambukizwa virusi vya Covid-19 barani Afrika.

Ugonjwa wa corona umeenea katika nchi 50 barani. Kwa ujumla, watu 5,413 wameambukizwa.

Mpaka sasa hakuna taarifa zozote za maambukizi nchini Lesotho, Sudani Kusini, visiwa Sao Tome na Principe, comoro na Malawi.

Hapo jana eno lililojitangazia uhuru wake Somaliland lilithibitisha kuwepo na maambukizi ya watu wawili. Redio Kulmiye imesema mmoja kati ya walioambukizwa ni raia wa China aliyekuwa akiishi katika mji wa Berbera. Mwingine ni raia wa Somalia ambaye hivi karibuni alirejea kutoka nchini Uingereza.

Somaliland imesambaza vikosi vyake mitaani na kupiga marufuku utafunaji wa mirungi mitaani kuepuka kusambaa kwa virusi.

Afrika Kusini ina idadi kubwa ya maambukizi,ikiwa imefikia 1,353, watu saba wakiwa wamepoteza maisha.

Watu 11 wamethibitishwa kuambukizwa virusi vya corona tangu jana nchini Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo na kufanya idadi ya walioambukizwa kufikia 109 na vifo vinane.

Wangojwa wa tatu hadi sasa wameripotiwa kupona lakini mgojwa wa kwanza hadi sasa yungali hospitalini , serikali haijamruhusu kurejea nyumbani kwake.

Mashirika ya kiraia yamelaani serikali kupuuza kufuatilia kwa karibu utelekezaji wa maagizo ya kuepusha kuenea kwa virusi nchini.

Wiki jana, serikali ilitangaza kusitisha hatua yake ya kuzuia raia wa kinshasa kutoka nyumbani.

Miongoni mwa maagizo , Rais Felix Tshisekedi aliomba viongozi wa mitaa kuweka maji na sabuni barabarani,lakini hadi sasa vifaa hivyo vya kiafya bado havijasambazwa katika mitaa ya Kinshasa.
 CHANZO - BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com