Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akimkabidhi Mganga Mkuu Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile Methylated Sprit 'Sanitizer' ikiwa ni sehemu ya vifaa vyenye thamani shilingi milioni 10.7 kwa ajili ya kujikinga na kukabiliana na Maambukizi ya Virusi vya Corona wakati wa matibabu vilivyotolewa na wadau wa afya mkoa wa Shinyanga likiwemo shirika la Touch Foundation leo Jumatatu Aprili 6,2020 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akimkabidhi Mganga Mkuu Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile Methylated Sprit 'Sanitizer' ikiwa ni sehemu ya vifaa vyenye thamani shilingi milioni 10.7 kwa ajili ya kujikinga na kukabiliana na Maambukizi ya Virusi vya Corona wakati wa matibabu vilivyotolewa na wadau wa afya mkoa wa Shinyanga likiwemo shirika la Touch Foundation.
Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akimkabidhi Mganga Mkuu Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile, Sriex Premium Latex ikiwa ni sehemu ya vifaa vyenye thamani shilingi milioni 10.7 kwa ajili ya kujikinga na kukabiliana na Maambukizi ya Virusi vya Corona wakati wa matibabu vilivyotolewa na wadau wa afya mkoa wa Shinyanga likiwemo shirika la Touch Foundation.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack (katikati) akiwa ameshikilia Barakoa ' Mask' akiangalia pamba aliyokabidhi Mganga Mkuu Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile ikiwa ni sehemu ya vifaa vyenye thamani shilingi milioni 10.7 kwa ajili ya kujikinga na kukabiliana na Maambukizi ya Virusi vya Corona wakati wa matibabu vilivyotolewa na wadau wa afya mkoa wa Shinyanga likiwemo shirika la Touch Foundation. Kushoto ni Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Rose Malisa.
Mganga Mkuu Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile (kulia) akimwelezea Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack kuhusu vidonge vya Chlorine vilivyotolewa na wadau wa afya mkoa wa Shinyanga. Kushoto ni Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Rose Malisa.
Sehemu ya vifaa vyenye thamani shilingi milioni 10.7 kwa ajili ya kujikinga na kukabiliana na Maambukizi ya Virusi vya Corona wakati wa matibabu vilivyotolewa na wadau wa afya mkoa wa Shinyanga likiwemo shirika la Touch Foundation.
Sehemu ya vifaa vyenye thamani shilingi milioni 10.7 kwa ajili ya kujikinga na kukabiliana na Maambukizi ya Virusi vya Corona wakati wa matibabu vilivyotolewa na wadau wa afya mkoa wa Shinyanga likiwemo shirika la Touch Foundation.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akiangalia vifaa vyenye thamani shilingi milioni 10.7 kwa ajili ya kujikinga na kukabiliana na Maambukizi ya Virusi vya Corona wakati wa matibabu vilivyotolewa na wadau wa afya mkoa wa Shinyanga likiwemo shirika la Touch Foundation.
Mganga Mkuu Mkoa w Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile akiwashukuru wadau wa sekta ya afya waliochangia upatikanaji wa vifaa vyenye thamani shilingi milioni 10.7 kwa ajili ya kujikinga na kukabiliana na Maambukizi ya Virusi vya Corona wakati wa matibabu vilivyotolewa na wadau wa afya mkoa wa Shinyanga likiwemo shirika la Touch Foundation.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akiwashukuru wadau wa sekta ya afya waliochangia upatikanaji wa vifaa vyenye thamani shilingi milioni 10.7 kwa ajili ya kujikinga na kukabiliana na Maambukizi ya Virusi vya Corona wakati wa matibabu vilivyotolewa na wadau wa afya mkoa wa Shinyanga likiwemo shirika la Touch Foundation.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akiwashukuru wadau wa sekta ya afya waliochangia upatikanaji wa vifaa vyenye thamani shilingi milioni 10.7 kwa ajili ya kujikinga na kukabiliana na Maambukizi ya Virusi vya Corona wakati wa matibabu vilivyotolewa na wadau wa afya mkoa wa Shinyanga likiwemo shirika la Touch Foundation.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akisisitiza umuhimu wa kunawa muhimu kwa wananchi wa mkoa wa Shinyanga wakati akikabidhi vifaa vyenye thamani shilingi milioni 10.7 kwa ajili ya kujikinga na kukabiliana na Maambukizi ya Virusi vya Corona wakati wa matibabu vilivyotolewa na wadau wa afya mkoa wa Shinyanga likiwemo shirika la Touch Foundation.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akisisitiza umuhimu wa kunawa muhimu kwa wananchi wa mkoa wa Shinyanga. “Kunawa ni jukumu letu sote. Uwe mtoa huduma wa afya uwe mwananchi. Naweni mikono kwa sababu mikono haipungui nguvu kwa kunawa".
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack amekabidhi vifaa vyenye thamani shilingi milioni 10.7 kwa Mganga Mkuu Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile kwa ajili ya kuzigawa katika halmashauri za wilaya ili kujikinga na kukabiliana na Maambukizi ya Virusi vya Corona wakati wa matibabu vilivyotolewa na wadau wa afya mkoa wa Shinyanga likiwemo shirika la Touch Foundation.
Hafla fupi ya Makabidhiano ya vifaa hivyo imefanyika leo Jumatatu Aprili 6,2020 katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga.
Mkuu huyo wa mkoa amewashukuru wadau wote wa afya waliochangia kupatikana kwa vifaa hivyo wakiongozwa na Touch Foundation iliyotoa shilingi milioni 10.4 na wadau wengine walichangia shilingi 300,000/= na kufanikisha kupatikana kwa vifaa hivyo kwa ajili ya kujikinga na kukabiliana na Maambukizi ya Virusi vya Corona wakati wa matibabu.
“Tunawashukuru wadau wanaoshughulika na afua za afya katika mkoa wetu,nakumbuka siku ya Ijumaa wiki iliyopita tulikaa kikao cha pamoja nao na waliahidi,na mmoja kati ya wadau walioahidi moja kwa moja ni Touch Foundation tunawashukuru ahadi yao leo imetekelezeka kwa kuchangia shilingi milioni 10.4”,amesema Telack.
“Tunawashukuru sana Touch Foundation na wadau wengine naamini huko waliko wanaendelea kujikusanya kutusaidia ili kama mkoa tuweze kuhakikisha kuwa kama kutatokea mgonjwa yeyote basi tunaweza kumhudumia kwani lengo ni kumhudumia mgonjwa na tunamkinga mtoa huduma wetu kwenye vituo tulivyovitenga ili aweze kumhudumia mgonjwa lakini na yeye abaki salama”,amesema Telack.
Mkuu huyo wa Mkoa amewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari kwa kunawa mikono huku akibainisha kuwa serikali haitasita kuwachukulia hatua za kisheria wale wanaokaidi kufuata maelekezo ya kunawa mikono.
“Tumeshatoa elimu ya kutosha,hakuna mahali ambapo hatujapita,sasa ni wakati wa kuchukua hatua wale ambao kwa maksudi kabisa wanakataa kunawa tuchukue hatua,tupige faini na wale wanaokaidi kabisa tupeleke kituo cha polisi ili hatua nyingine zichukuliwe ili tuiache Shinyanga ikiwa salama na nchi kwa ujumla kutokana na Corona”,amesema Telack.
Mkuu huyo wa mkoa amesema kunawa mikono ni jukumu la kila mtu . “Kunawa ni jukumu letu sote. Uwe mtoa huduma wa afya uwe mwananchi. Naweni mikono kwa sababu mikono haipungui nguvu kwa kunawa. Na nyinyi watoa huduma naomba muwe mstari wa kwanza kuhakikisha kuwa mnapoingia pale mlangoni mnanawa mikono yenu muoneshe mifano ili wananchi waige kutoka kwenu”,amesema Telack.
“Kazi kubwa tuliyonayo ni kuhakikisha kwamba tunachukua tahadhari,tujikinge na tuwakinge wengine kwa kunawa mikono. Kwa Maafisa afya muda huu siyo wa kukaa maofisini,ni muda wa kupita kwenye maeneo ya kazi,kwenye ofisi zote,kwa wafanyabiashara kuhakikisha kuwa watu wote wananawa mikono” ,amesema Telack.
“Niwaombe sana watoa huduma kaeni tayari kwa chochote kitakachojitokeza kwa sasa tunamshukuru Mungu kwamba mkoa wetu bado upo salama lakini sisi siyo Kisiwa,pamoja na kuomba Mungu kaeni tayari,jiandaeni kwa ajili ya chochote kile kitatokea,muwe tayari kwenda kutoa huduma na sisi tutaendelea kutafuta kila njia kupata Protective Gears ili muweze kuwa salama wa mnapokwenda kutoa huduma”,ameongeza Telack.
Mganga Mkuu Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile amevitaja miongoni mwa vifaa vilivyotolewa na wadau wa sekta ya afya mkoani Shinyanga kuwa ni Surgical gloves, Non Sterile gloves,Barakoa ‘Mask’,Methylated Spirit, vidonge vya Chlorine na pamba.
“Wiki iliyopita tulikaa na wadau wa sekta ya afya mkoa wa Shinyanga na kwa pamoja wakakubaliana kwamba watachangia na kusaidia mkoa wa Shinyanga katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Corona. Siku hiyo tulipata mchango wa mtu mmoja mmoja ukiachilia mbali mashirika yao waliweza kuchangia kiasi cha shilingi 300,000/= na kiasi hicho tumeweza kununua vifaa na tunaye mdau Touch Foundation ambaye ametoa pia vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 10.4”, amesema Dkt. Ndungile.
Amesema vifaa vilivyopatikana vitagawiwa katika halmashauri zote za wilaya mkoani Shinyanga.