FISI ALIYEVAMIA KUNDI LA MBUZI AJERUHI WATU WAWILI KAHAMA


Na Salvatory Ntandu - Kahama
Wakazi wawili wa Kijiji cha Ngogwa halmashauri ya Mji wa Kahama mkoani Shinyanga wamenusurika kufa baada ya kushambuliwa na  Fisi wakati wakijaribu kumfukuza fisi huyo aliyekuwa amevamia kundi la mbuzi katika kijiji hicho.


Akizungumza na waandishi wa Habari leo Aprili 19, 2020 Afisa mtendaji wa Kata hiyo Upendo Shirima amesema tukio hilo limetolea  leo saa mbili asubuhi ambapo Fisi  huyo  alivamia zizi la Mbuzi  kabla ya wananchi kuanza kumpiga na ndipo alipowajeruhi sehemu za mikononi wananchi hao ambao wamepelekwa katika hospitali ya halmashauri ya mji wa Kahama kwa matibabu.

Amewataja walioshambuliwa Fisi na huyo kuwa ni Pamoja na Donald Simoni (27) na Furaha Ngusa (46) na ameiomba Wizara ya Maliasili kutenga siku maalumu ili kwenda kuwawinda fisi hao ambao wamekuwa ni wengi kwa wakati huu.

“Tunaomba tu watu wa maliasili watusaidie kufanya oporesheni  juu ya wananyama hao maana kutokana na mvua hizi Maji yameingia kwenye mapango yao hali ambayo inawafanya waje kwenye makazi ya watu”,amesema Shirima.

Amesema kuwa watu wameanza kupata hofu kutokana na wananyama hao kuanza kuvamia nyakati za mchana kwani walizoea kuwaona wakivamia mifugo wakati za usiku.

Diwani wa Kata ya Ngogwa  Kamuli Mayuga amesema  baada ya kuwafikisha hospitalini wamepatiwa matibabu kwa kushonwa nyuzi kwenye majereha na kuruhusiwa kuerejea nyumbani huku akiwataka wananchi waendelee kuchukua tahadhari.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post