Muonekano wa Hoteli Tanga Beach Resort
Muonekano wa Hoteli Tanga Beach Resort
MENEJIMENTI ya uongozi wa hoteli yenye hadhi ya nyota tano ya Tanga Beach resort iliyoko jiji Tanga imelazimika kufunga hotel hiyo ili kuunga mkono jitihada za serikali za kuzuia mikusanyiko ili kujikinga na ugonjwa wa virusi vya Corona vinavyotokisa dunia kwa sasa.
Akitoa tamko hilo mbele ya waandishi wa habari Meneja wa hotel hiyo Joseph Ngonyo alisema kuwa wameamua kufunga kutokana na mlipuko wa ugonjwa huo hapa Tanzania pamoja na na kudhibiti mkusanyiko wa watu
Alisemam kuwa awali tayari biashara ya hotel ilianza kususasua kutokana na uwepo wa ugonjwa huo hivyo kulazima kufunga ili kuzuia mkusanyiko wa waty hasa katika kipindi hiki cha kuelekea katika msimu wa sikukuu.
“Dunia sasa hivi na hata nchini kwetu kumekuwa na tatizo la gonjwa la Corona hivyo tumeamua kusitisha huduma ili kuunga mkono kauli ya serikali ya kuzui mkusanyiko wa wau wengi pamoja hivyo ili kuwathibiti tumelazimika kufunga hotel hiyo”alisema Ngonyo.
Aidha aliwataka wananchi kuacha dhana potofu ambazo zimeanza kusambaa katika mitandao ya kijamii na kwamba wameamua kuunga mkono juhudi za serikali hivyo shughuli za hotel zinatarajiwa kuanza tena mwishoni mwa mwezi Mei.
Kwa upande wake mmoja wa wafanyakazi katika hotel hiyo Hadija Ramadhani alisema kuwa wamelazimika kuunga mkono maagizo ya serikali ili kupunguza maambukizi kwa wafanyakazi pamoja na wananchi ambao wanaweza kufika katika hotel kwa ajili ya kupata huduma.
“Tunaomba watu waachane na habari za mitandao kwani zinatuchafua lakini lengo letu ni kuhakikisha usalama wa wafanyakazi wetu pamoja na wateja ambao wanakuja kupata huduma katika hotel yety”alisema Ramadhani
Naye kwa upande wake mfanyakazi wa Hoteli hiyo kitengo cha mapokezi Khadija Mcharo alisema kwa sasa huduma zao wamesitisha kutokana na uwepo wa virusi vya Corona na wanaiunga mkono serikali katika juhudi zake za kupambana kupunguza maambukizi hayo.