Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

IGP SIRRO: WANAOTUMIA MITANDAO YA KIJAMII KUPOTOSHA KUHUSU CORONA WACHUKULIWE HATUA KALI ZA KISHERIA


Mkuu wa Jeshi la polisi nchini IGP Simon Sirro   ameagiza kuchukuliwa  hatua kali za kisheria baadhi ya watu wanaotumia mitandao kwa nia yao ovu ya kupotosha kuhusu ugonjwa wa Corona


“Watu wa mitandao ni sumu sana…hasa wanapoitumia vibaya…maelekezo kwa makamanda hawa ni kuhakikisha kwamba akijitokeza mtu mmoja au kikundi cha watu wakafanya haya wanayoyafanya kwa ajili ya kuwaletea watanzania hofu…tuwashughulikie vizuri sana…” - Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro.

==>>Msikilize hapo chini


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com