DEREVA BODABODA MWENYE VIRUSI VYA CORONA AKAMATWA AKISAFIRISHA JENEZA FEKI

Polisi nchini Kenya imemkamata dereva aliyekuwa na virusi vya corona pamoja na abiria watatu waliojidai kuwa waombolezaji wanaoelekea kwa mazishi.

Watatu hao waliokuwa wamesafiri zaidi ya kilomita 370 kutoka kutoka Nairobi wakiwa na jeneza bila maiti walikamatwa katika jimbo la Homa Bay magharibi mwa Kenya.

Tukio hilo la kushangaza liliangaziwa na Waziri wa Afya wa Kenya Bw. Mutahi Kagwe ambaye pia alithibitisha kuwa kundi hilo lilifanikiwa kuhadaa polisi kwa kutumia jeneza tupu na kupita vizuizi kadhaa njiani.

Aliongeza kuwa dereva huyo ametengwa na abiria wake kuwekwa karantini.

Karibu wiki mbili zilizopita serikali ya Kenya ilitangaza hatua kali za kudhibiti watu kuingia na kutoka katika mji mkuu wa Nairobi pamoja na majimbo menginine matatu ambayo yanasadikiwa kuwa na viwango vya juu vya maambukizi ya ugonjwa wa Covid-19.

Waziri wa Afya alisema serikali inachunguza madai kwamba baadhi ya watu wanatoa hongo kwa polisi wanaolsimamia vizuizi vya barabarani.

Malori yanayoenda safari za mwendo mrefu pia pia zinachunguzwa kutokana na madai ya kuwasafirisha watu kinyemela kutoka jijini Nairobi

Kufikia sasa Kenya ina jumla ya wagonjwa 262 wa covid-19 baada ya watu 16 wapya kuthibitishwa kuwa na virusi Jumamosi.
Chanzo - BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post