Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Jeshi la polisi mkoani Dodoma limemkamata mwanamke mmoja Grace Rauwo Miaka 31 mkazi wa MTONI KWA AZIZI ALLY Jijini Dar Es Salaam kwa kosa la wizi kwa njia ya mtandao na akiwa na gari lenye namba za usajili T.745 DSS aina ya TOYOTA CROWN rangi nyeupe alilokuwa anatumia katika uhalifu na likidhaniwa kuwa ni la wizi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo April,9,2020 jijini Dodoma Kamanda wa Polisi mkoani hapa SACP Gilles Muroto amebainisha kuwa ,Mwanamke huyo huwa anafanya uhalifu huo na timu ya wenzake wanaojihusisha na wizi wa fedha kwa njia ya mtandao na wamejisajili kama mawakala .
Kamanda Muroto amesema wahalifu hao wamechonga laini za simu ,wanaingilia mifumo ya neno la siri za wateja na kuwaibia fedha ambapo kabla ya kukamatwa waliiba fedha kwa njia ya mtandao Tsh.Milioni 27 na kugawana fedha hizo na yeye kuamua kununua gari hilo lenye Namba za usajili T.745 DSS ambalo pia wanalitumia kufanya uhalifu katika mikoa mbalimbali.
Katika tukio jingine Kamanda Muroto amebainisha kuwa huko mtaa wa Chinyoya kata ya Kilimani jijini Dodoma katika msako na kwa msaada wa askari wa jeshi la wananchi Tanzania[JWTZ]aliweza kumkamata Godfrey Francis Shirima [22]mpiga picha na mkazi wa Image jijini Dodoma akiwa na silaha Bastola aina ya Browning yenye Na.016975 akiimiliki kinyume cha sheria na kuitumia katika uhalifu na atafikishwa mahakamani muda wowote.
Aidha ,Kamanda Muroto ameendelea kufafanua kuwa ,tarehe 7/04/2020 kijiji cha Chilungulu tarafa ya Bahi mkoani Dodoma aliuawa Mwalimu Eradius Mgaya kwa kupigwa na kitu chenye ncha kali na kutupwa kwenye shamba la shule baada ya kuviziwa njiani wakati akirejea nyumbani kwake ambapo watu watano wamekamatwa kwa tuhuma hizo.
Kamanda Muroto ametoa rai kwa wananchi wa Dodoma na watu wote wanaochukia uhalifu kushirikiana na jeshi hilo kwa kutoa taarifa za uhalifu .
Social Plugin