Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

JESHI LA POLISI KANDA MAALUMU YA DAR ES SALAAM LAPIGA MARUFUKU MIKUSANYIKO BAHARINI, BAA


Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limepiga marufuku mikusanyiko katika fukwe za bahari na kwenye baa katika kipindi chote cha sikukuu za pasaka.


Akizungumza na waandishi wa habari jsn Alhamisi Aprili 9, 2020 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum, Lazaro Mambosasa amewataka wananchi wote kuepuka mikusanyiko isiyokuwa ya lazima na kuendeleza na jitihada za kujikinga na virusi vya corona.

“Katika kipindi chote cha pasaka polisi Kanda Maalum imejipanga hukakikisha hakuna uhalifu, vurugu na mikusanyiko isiyokuwa ya lazima inafanyika ikiwa ni maelekezo ya Serikali ya kujikinga na maambukizi ya corona,” amesema Mambosasa.

Vilevile, jeshi hilo limewataka madereva wa pikipiki walioruhusiwa kuingia katikati ya jiji kufuata sheria kwa kuvaa kofia ngumu na kuacha kupita barabara zilizokatazwa.

Aprili Mosi, 2020, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda aliruhusu bodaboda na bajaji kuingia katikati ya jiji ili kupunguza kero ya usafiri uliotokana na daladala kutakiwa kupakiwa abiria kulingana na idadi ya viti ‘level seat’.

“Fursa waliyoipata wataipoteza wenyewe wameruhusiwa wanakuja na tabia zao za kuendelea kukiuka na kuwa wakaidi, tumejipanga vizuri kuhakikisha kwamba yeyote atakayeenda kinyume tunamchukulia hatua,” amesema

“Tunawashukuru waliotii agizo la Serikali la kupakia abiria kulingana na idadi ya viti vilivyopo ndani ya gari (level seat) kwa watakaokaidi agizo hilo sheria itafuata mkondo wake.”

Ameongeza kuwa jeshi hilo limejipanga vizuri kwa kutumia doria za askari wa miguu, magari, pikipiki, mbwa na farasi kuhakikisha maeneo yote yanakuwa salama.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com