Mkazi wa Kata ya Wailes, Halmashauri ya Manispaa ya Lindi, Selemani Hassani (29) amehukumiwa kifungo cha maisha gerezani,baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mtoto wa miaka 8.
Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu mkazi mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Lindi, Maria Batraine, baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa Mashitaka.
Kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo, Hakimu Batraine alimuuliza mshitakiwa iwapo ana sababu za msingi itakayoiwezesha Mahakama isimpe adhabu kali kutokana na kosa linalomkabiri mbele yake,ambapo aliomba aonewe huruma kwani ni mkosaji wa mara ya kwanza na pia anayofamilia inayomtegemea.
"Naiomba Mahakama yako tukufu naomba inionne huruma kwani shetani wa mapenzi alinipitia na sasa najutia kosa langu" amedai Selemani.
Hakimu Betraine akitoa hukumu katika kesi hiyo namba 08/2020, amesema amesikia maombi ya pande zote mbili,lakini kutokana na kubanwa na Sheria kupitia vifungu 130 kifungu kidogo cha kwanza fungu la pili kipengele (e) pamoja na 131 fungu dogo la (1) na (3) alimuhukumu kutumikia kifungo cha maisha Gerezani.
Social Plugin