Jimbo la New York nchini Marekanai sasa lina visa vingi vya virusi vya corona zaidi ya taifa lolote duniani , kulingana na takwimu mpya.
Serikali imethibitisha kwamba idadi ya visa vya ugonjwa huo imeongezeka kutoka 10,000 siku ya Alhamisi hadi 159, 937 na kuiweka mbele ya Uhispania ilio na visa 153,000 na Itali ilio na visa 143,000.
China ambapo virusi hivyo vilianza mwaka uliopita iliripoti visa 82,000. Marekani yote imerekodi visa 462,000 na takriban vifo 16,500.
Kote duniani kuna takriban visa milioni 1.6 na vifo 95,000.
Huku Jimbo la New York likiongoza ulimwengu katika visa vya maambukizi , takriban watu 7000 wamefariki katika mji huo , ikiwa nyuma ya Uhispania ilio na vifo 15,500 na Itali ilio na 18,000 ikiwa ni mara mbili ya vifo vya China 3,300.
Social Plugin