Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Marin Hassan Marin wa TBC amefariki dunia leo Aprili Mosi asubuhi katika Hospitali ya Jeshi Lugalo, jijini Dar es Salaam.
Kabla ya kufanya kazi TBC Marin alifanya kazi Televisheni ya Zanzibar (TVZ) na ni miongoni mwa waandishi walionesha kipaji mapema wakati wakianza kazi ya uandishi wa habari, Marin pia ni katika waanzilishi wa kipindi cha Redio cha Mawio kilichokuwa zikikirushwa na Sauti ya Tanzania Zanzibar (STZ) ambacho kinaendelea hadi leo kwenye Shirika la Utangazaji la Zanzibar (ZBC).
Mwili wa Marehemu utapelekwa Zanzibar kwa mazishi.
R.I.P Marin
Social Plugin