Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewatakia heri Watanzania wote katika kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 56 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar huku akiwataka kutumia siku ya kesho Aprili 26,2020 kuutafakari Muungano ulioasisiwa na Viongozi wakuu Baba wa Taifa, Hayati Mwl Julius Kambarage Nyerere na Hayati Sheikh Abeid Amani Karume pamoja na kumuomba Mwenyezi Mungu aepushe janga la Ugonjwa wa Corona.
Aidha katika kuadhimisha miaka 56 ya Muungano,Rais Magufuli ametoa msamaha kwa jumla ya wafungwa 3,973 ambapo kati yao wafungwa 3,717 wamesamehewa vifungo vyao na wafungwa 256 waliokuwa wanakabiliwa na adhabu ya kunyongwa hadi kufa wamebadilishiwa adhabu hiyo.
Social Plugin