Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki wa Watu takribani 18 waliopoteza maisha katika ajali ya Barabarani iliyotokea leo April 15, saa 12:55 asubuhi Kijiji cha Kilimahewa Kaskazini,Mkuranga,Pwani ikihusisha basi dogo (Coaster) lililokuwa likitoka Mkuranga kwenda Dar es salaam kugongana uso kwa uso na lori la mizigo lililokuwa likitoka Dar es salaam kwenda Mikoa ya Kusini.
“Nawaombea Familia za Marehemu wote, Ndugu, Jamaa na Marafiki kuwa na moyo wa uvumilivu na ustahimilivu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi, kuwapoteza Watanzania wenzetu kwa idadi kubwa namna hii inaumiza sana”,amesema Rais Magufuli.
Social Plugin