KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Tanga Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi (ACP) Blasius Chatanda akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali
KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Tanga Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi (ACP) Blasius Chatanda akiwaonyesha waandishi wa habari vitu ambavyo vimekamatwa wakati wa opeseheni hiyo
Camera ambazo pia zimekatwa wakati wa operesheni hiyo
KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Tanga Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi (ACP) Blasius Chatanda ametoa onyo kali kwa wezi wanaovunja nyumba za watu na kuiba mali kwa kuwataka waache mara moja tabia hiyo kabla hawajawafinyanga finyanga.
Chatanda aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema kwamba awali kulikuwa kumeibuka wimbi la uvunjaji wa nyumba hali ambayo iliwalazimu kuanzisha operesheni kabambe ya kuwasaka ili kuhakikisha wananchi wanaishi kwa amani.
Alisema kwamba katika operesheni hiyo walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa 8 ambao kwa sasa wapo mahabusu ambapo walikamatwa wakiwa na vitu mbalimbali ambavyo waliviiba kwenye maeneo mbalimbali Jijini Tanga.
Kamanda Chatanda alitaja vitu ambavyo vilikamatwa kuwa ni Televison ya Flat Screen 7zenye ukubwa wa tofauti kuanzia nch 50 hadi 21 ambazo zinadaiwa ziliibiwa kwenye baadhi nyumba za kulala wageni zilizopo Jijini Tanga.
Aidha alisema pia katika operesheni hiyo waliwakamata vitu vingine ikiwemo Kompyuta mpakato 16,simu za mkononi 7 ambapo baadhi ya vitu hivyo viliibiwa kwenye nyumba za kulala wageni.
“Tunaomba walioibiwa waje watambue mali zao kama ni miongoni mwa zilizokamatwa huku akisisitiza kwamba msako huo ni endelevu na hakuna mtu ambaye hatabaki salama “Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga.
Kamanda huyo alisema kwamba msako huo ni endelevu na hakuna mtu ambaye atabaki salama huku akieleza kwamba kwa waliozoea kuiba watafute kazi nyengine za kufanya kwa sababu wakikamatwa watawafinyangafinyanga mpaka wasahau njia walizokujia.
Social Plugin