SUDAN KUSINI YATHIBITISHA KISA CHA KWANZA CHA VIRUSI VYA CORONA

Sudan Kusini imeripoti kisa chake cha kwanza cha virusi vya Corona. 


Nchi hiyo ni moja ya nchi za mwisho za Afrika kuthibitisha uwepo wa ugonjwa wa COVID 19 ndani ya mipaka yake. 

Akizungumza na waandishi habari mjini Juba makamu wa rais Riek Machar amesema mtu wa kwanza alieambukizwa virusi hivyo ni mwanamke aliye na miaka 29 aliyeingia Sudan Kusini akitokea Uholanzi kupitia Ethiopia tarehe 28 Februari. Bado uraia wake haujatajwa. 

Taarifa kutoka kikosi cha amani cha Umoja wa Mataifa nchini humo UNMISS zinasema mwanamke huyo ni mtumishi wake. 

Machar amesema Wizara ya afya kwa kushirikiana na shirika la afya duniani WHO pamoja na shirika la kudhibiti magonjwa ya kuambukiza wanawafuatilia wote waliokaribiana na mwanamke huyo.

 Sudan Kusini tayari imefunga migawaha, vilabu vya usiku na maduka isipokuwa yale yanayouza vyakula na kuwahimiza watu kuzingatia kanuni za kujitenga.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post