Rais wa Marekani Donald Trump ameungana na Viongozi wengine Duniani, kutoa pole kwa swahiba wake, Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson kutokana na kuugua corona.
"....tumehuzunika kusikia ameingizwa ICU,Marekani inamuombea, tumewasiliana na Madaktari wake kuona kama tunaweza kusaidia"
Waziri Mkuu Johnson alipelekwa hospitali na kulazwa baada ya hali yake kuzidi kuwa mbaya kutokana na kuambukizwa Virusi vya Corona.
Kansela wa Ujerumani Angela merkel na rais wa Marekani Donald Trump ni miongoni mwa viongozi wa ulimwengu waliotuma salamu za kumtakia afya Waziri mkuu wa Uingereza.
Rais wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen amemtumia salamu waziri mkuu Johnson na amemtakia kupona haraka.
Naye rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema anasimama pamoja na bwana Johnson, familia yake na watu wa Uingereza katika wakati huu mgumu.
Mkurugenzi mkuu wa shirika la afya duniani WHO bwana Tedros Adhanom Ghebreyesus amemtumia kiongozi huyo wa Uingereza salamu za dhati wakati anapopambana na maambukizi ya virusi vya Corona.