Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akizungumza leo Ijumaa Aprili 10, 2020 katika kikao kazi chake na waandishi wa habari kilicholenga kujadili masuala mbalimbali ya ulinzi na usalama kilichofanyika katika Hoteli ya Travellers mjini Shinyanga - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog.
Jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga limeahidi kuendelea kushirikiana na Vyombo vya Habari kuhakikisha vitendo vya uhalifu ikiwemo mauaji,ajali za barabarani na ukatili wa kijinsia hususani mimba na ndoa za utotoni vinatokomezwa mkoani humo.
Hayo yamesemwa leo Ijumaa Aprili 10,2020 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba katika kikao kazi chake na waandishi wa habari kilicholenga kujadili masuala mbalimbali ya ulinzi na usalama kilichofanyika katika Hoteli ya Travellers mjini Shinyanga.
Kamanda Magiligimba amesema suala la ulinzi na usalama ni jukumu la kila mtu katika jamii huku akibainisha kuwa Waandishi wa habari wanayo nafasi kubwa zaidi kuielimisha jamii kuachana na vitendo viovu ndiyo maana Jeshi la polisi limekuwa likishirikiana bega kwa bega na waandishi wa habari kuhakikisha vitendo hivyo vinatokomezwa.
“Naomba waandishi wa habari tuendelee kushirikiana katika kuufanya mkoa wetu unakuwa mahali salama pa kuishi kwa kuhakikisha tunapunguza ajali za barabarani,mauaji kuepuka vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto”,amesema Kamanda Magiligimba.
Katika hatua nyingine ameitaka jamii kuachana na tabia ya kupeleka watoto wa kike/wasichana wadogo kwa waganga wa kienyeji kwenda kuoshwa dawa za mvuto/nyota maarufu ‘Samba’ ili wapendwe na wanaume kwani inachangia kuwepo kwa matukio ya mimba na ndoa za utotoni.
"Mkoa wa Shinyanga ulikuwa unakabiliwa na matukio ya mauaji ya wazee na watu wenye ualbino lakini sasa yamepungua kwa asilimia kubwa na kubaki tatizo la mimba na ndoa za utotoni ambalo linasababishwa na mila na desturi za kuogesha watoto wao wa kike dawa za mvuto wa mapenzi hasa katika wilaya ya Kishapu",amesema Magiligimba.
Amewaomba waandishi wa habari kushirikiana na Jeshi la polisi kwa kuandika habari ambazo zitatoa elimu kwa wazazi na walezi kuachana na mila potofu za kuogesha watoto wao wa kike dawa za mvuto wa mapenzi ili kutokomeza mimba na ndoa za utotoni mkoani Shinyanga.
Kamanda Magiligimba ametumia fursa hiyo kuwasihi wakazi wa Shinyanga kuzingatia maagizo ya Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto kuhusu Ugonjwa wa Corona ikiwemo kuepuka, Mikusanyiko isiyo ya lazima, kuepuka kukumbatiana , kunawa mikono kwa maji na sabuni mara kwa mara na kutumia Vitakasa Mikono 'Sanitizer'.
Kwa upande wake, Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Shinyanga SP Davis Msangi amewashukuru wadau mbalimbali wa masuala ya ulinzi na usalama kwa kushirikiana na jeshi la polisi kupunguza matukio ya mauaji ambapo katika Kipindi mwezi Januari hadi Machi 2020 kuna matukio 6 yametokea ukilinganisha na matukio 23 yaliyotokea Mwezi Septemba hadi Desemba 2019.
- Naye Mkuu wa Kikosi Cha Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga ASP Africanus Sulle amesema katika Kipindi hiki ambapo kuna Ugonjwa wa Corona, Jeshi la polisi limeendelea kutoa elimu kwa waendeshaji wa vyombo vya barabarani yakiwemo magari kuhakikisha hawajazi abiria kupita kiasi ili kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa wa Corona.
“Tunaendelea kukabiliana na ujazaji abiria kwenye magari yanayoingia mjini na yanayokwenda vijijini ili kukabiliana na ugonjwa wa Corona. Kwa upande wa magari madogo mfano Hiace tunaondoa viti vya nyuma ya dereva ili abiria wasiangaliane”,ameeleza Sulle.
Hata hivyo amesema jeshi la polisi halitasita kuwachukulia hatua za kisheria madereva bodaboda wanaoendesha kwa mwendo kasi Mjini Shinyanga huku akibainisha kuwa wanaendelea kutoa elimu kwa waendesha bodaboda kupitia kwenye vituo vyao kuzingatia sheria za usalama barabarani na kuhakikisha wananawa mikono kwa maji tiririka na sabuni na kutumia Sanitizer.
“Barabara kuwa salama ni lazima,nami nitahakikisha nasimamia Sheria na kanuni za usalama barabarani ili kuhakikisha tunapunguza ajali za barabarani ambazo zinasababisha vifo,ulemavu na uharibifu wa mali”,ameongeza Sulle.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akizungumza leo Ijumaa Aprili 10,2020 katika kikao kazi chake na waandishi wa habari kilicholenga kujadili masuala mbalimbali ya ulinzi na usalama kilichofanyika katika Hoteli ya Travellers mjini Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akizungumza leo Ijumaa Aprili 10,2020 katika kikao kazi chake na waandishi wa habari kilicholenga kujadili masuala mbalimbali ya ulinzi na usalama.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akizungumza leo Ijumaa Aprili 10,2020 katika kikao kazi chake na waandishi wa habari kilicholenga kujadili masuala mbalimbali ya ulinzi na usalama.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akizungumza leo Ijumaa Aprili 10,2020 katika kikao kazi chake na waandishi wa habari kilicholenga kujadili masuala mbalimbali ya ulinzi na usalama.
Kikao cha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba na waandishi wa habari kikiendelea.
Katikati ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akizungumza leo Ijumaa Aprili 10,2020 katika kikao kazi chake na waandishi wa habari kilicholenga kujadili masuala mbalimbali ya ulinzi na usalama. Kulia ni Mkuu wa Kikosi Cha Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga ASP Africanus Sulle , Kushoto ni Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Shinyanga SP Davis Msangi.
Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Shinyanga SP Davis Msangi akizungumza katika kikao cha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba na waandishi wa habari kilicholenga kujadili masuala mbalimbali ya ulinzi na usalama.
Mkuu wa Kikosi Cha Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga ASP Africanus Sulle akizungumza katika kikao cha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba na waandishi wa habari kilicholenga kujadili masuala mbalimbali ya ulinzi na usalama.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Social Plugin