Muungano wa klabu za waandishi wa habari Tanzania (UTPC),umetangaza mpango wa kugawa vifaa maalumu vya kujikinga na ugonjwa wa Covid 19 kwa klabu zote za waandishi wa habari Tanzania.
Hayo yamesemwa na Rais wa UTPC bwana Deogratius Nsokolo kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo April 25 Jijini Mwanza, kwenye ofisi za umoja huo.
Nsokolo amebainisha kuwa, utekelezaji wa mpango huo ni matokeo ya tathimini ya usalama kwa waandishi uliofanywa na UTPC na kubaini uwepo wa changamoto za vifaa kwa waandishi wa habari Nchini.
Nsokolo amebainisha kuwa klabu zote ishirini na nane zitapatiwa vifaa vya kujikinga, ikiwemo barakoa, vitiririsha maji na vitakasa mikono.
Pia UTPC imeiomba serikali na wadau wengine wa kimaendeleo Nchini kuliingiza kundi la waandishi wa habari kwenye migao ya vifaaa vya kujikinga na Corona vinavyotolewa wakati huu, kwa kuwa uhitaji wa vifaa kwa kundi hilo ni mkubwa zaidi.
Pia UTPC imewaomba waandishi kuzingatia maelekezo ya kujikinga yanayotolewa na wataalamu wa Afya Nchini ili waendelee kufanya kazi zao wakiwa salama.
Kundi la waandishi wa habari ni moja kati ya makundi yanayofanya kazi kwenye mazingira ya hatari na hivyo kuwa na mikakati ya kujilinda ni mushimu.
Edwin Soko
Watetezi Tv
Mwanza
25.04.2020
Social Plugin