Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa kushoto akiwa na Mganga Mkuu wa Jiji la Tanga (CMO) kulia wakiwa stendi za mabasi Jijini Tanga wakiangalia namna ya
utekelezaji wa maagizo ya wataalamu wa afya namna ya kuchukua hatua za kukabiliana na tahadhari za ugonjwa wa Corona.
MKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa kulia akiteta jambo na Afisa Mtendaji wa Kata ya Ngamiani Kati wakati wa ziara yake
VIBAKA wametumia fursa ya uwepo wa ugonjwa wa Corona kuiba Koki zilizowekwa kwenye ndoo za maji kwenye stendi ya mabasi madogo ya ngamiani Jijini Tanga na hivyo kusababisha kukosekana kwake na hivyo kuleta usumbufu mkubwa kwa watumiaji.
Hayo yalibainishwa na Msimamizi wa magari madogo maarufu Daladala kwenye stendi hiyo Ally Kibaya wakati wa ziara ya Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa wakati alipokwenda kuangalia utekelezaji wa maagizo ya wataalamu wa afya namna ya kuchukua hatua za kukabiliana na tahadhari za ugonjwa wa Corona.
Koki hizo na ndoo zilitolewa na chama cha wamiliki wa mabasi madogo (Taremia) na Chama cha Wamiliki wa Mabasi Makubwa (Taboa) kuona namna ya kuweza kupambana na ugonjwa wa Corona walipotoka hapo Taremea wakanunua ndooo za kutosha na kutafuta fundi wa kuweka koki na kufanya uzinduzi ambapo kila stendi waliweka ndoo sita kwa ajili ya kuwekwa kwenye maeneo ya stendi hiyo ya mabasi ili kuwawezesha wananchi kuweza kunawa na vitakasa mikono.
Alisema kwamba hali hiyo imewapa wakati mgumu kwani kuibiwa kwa koki hizo kumepelekea maji kushindwa kukaa kwenye ndoo na hivyo abiria kukosa eneo la kunawia mikono ili kuweza kujikinga na ugonjwa huo.
“Uibaji wa koki hizo umesababisha ndoo kushindwa kukaa na maji na hivyo kuwaweka kwenye wakati mgumu huku wakimuomba mkuu wa wilaya kulishughulikia tatizo hilo ambalo linaweza kuleta athari”Alisema Msimamizi huyo.
Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa alisema wizi huo ni hujuma dhidi ya mapambano dhidi ya ugonjwa wa Corona ambapo alionya tabia hiyo na kiwataka wanaohusika kutokurudia na vitendo vya namna hiyo.
Aliita mkutano wa mabasi na Alisema kwamba mtu anayekwamisha mapambano hayo dhidi ya Corona hatutawanyamazia watakaobainika wataendelea kuchukuliwa hatua kali kwani wanadhoofisha juhudi za kupambana na ugonjwa huo ambao kwa sasa unatikisha dunia.
Mkuu huyo wa wilaya alisema katika vita dhidi ya mapambano ya ugonjwa huo tusifanya hujuma hasa kwa vile vitu ambavyo vinatolewa na watu kwa ajili ya kukabiliana na janga hili ambapo alisema kitendo hicho hakina tofauti na laana
“Watu wamechangishana kutusaidia kwa lengo la kuweka usafi hasa kwenye maeneo ya stendi lakini unakuja kuhujumu koki hilo sio suala nzuri hivyo niwatake muacha mara moja tabia hiyo kwani tutakaowabaini watachukuliwa hatua”Alisema
Social Plugin