Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WAGONJWA WA CORONA KENYA WAFIKA 296....NI BAADA YA WENGINE 15 KUONGEZEKA LEO


Wizara ya Afya nchini Kenya imetangaza ongezeko la wagonjwa 15 wapya waliothibitishwa kuwa na virusi vya corona na kufikisha 296 jumla ya watu wanaougua Covid-19 nchini humo.

Wagonjwa 11 ni raia wa Kenya na wanne ni raia wa kigeni ambao walikuwa miongoni mwa watu 545 waliofanyiwa vipimo vya kubaini ikiwa wana virusi vya ugonjwa huo katika kipindi cha saa 24 zilizopita.

Akizungumza na wanahabari leo Jumanne, Katibu Mkuu wa Afya nchini humo Dkt. Mercy Mwangangi amesema visa saba vya maambukizi vilirekodiwa Mombasa pwani ya Kenya, sita mjini Nairobi na viwili katika mji wa kaskazini mashariki wa Mandera.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com