Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametangaza maambukizi mapya ya watu 11 ya ugonjwa wa Corona nchini humo, wakiwemo baadhi ya wanakwaya wa kwaya maarufu nchini humo 'Watoto Children's Choir.
Kupitia matangazo ya televisheni, alisema kuwa wagonjwa wote wapya walikuwa karantini baada ya kurejea kutoa ughaibuni , ingawa hakueleza afya zao zikoje kwa sasa na walikuwa wametoka taifa gani.
Mara nyingi kwaya hiyo huwa inatumbuiza katika nchi za ughaibuni kama Marekani, Canada na Uingereza.
Mpaka sasa Uganda imethibitisha kuwa na wagonjwa wa Corona 44.
Social Plugin