WAZIRI MKUU ALIYEMNG'OA MUAMMAR GADDAFI AFARIKI DUNIA KWA CORONA

Aliyekuwa Waziri Mkuu wa mpito nchini Libya, Mahmoud Jibril,  amefariki dunia baada ya kupata maambukizi ya virusi vya Corona.


Imeelezwa kuwa kiongozi huyo wa zamani aliyeongoza mapinduzi yaliyomtoa madarakani marehemu Muammar Gaddafi mwaka 2011 alilazwa hospitali baada ya kupata mshtuko wa moyo na siku tatu baadaye, aligundulika kuwa na ugonjwa wa COVID-19 na kuwekwa karantini.

Mkurugenzi wa Hospitali ya Ganzouri iliyopo mjini Cairo, Hisham Wagdy, amesema Jibril alifikishwa hospitalini hapo Machi 21, 2020,  na alithibitishwa kuwa na virusi hivyo siku chache baadaye.

Ameeleza kuwa kiongozi huyo alikuwa akiendelea vizuri lakini hali yake ilibadilika ghafla na kusababisha kifo chake.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post