Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson ametolewa katika Chumba cha Uangalizi Maalum (ICU) na kuhamishiwa wodini huku bado akiendelea kuwa chini ya uangalizi maalum.
Taarifa iliyotolewa na Ofisi yake imeeleza kuwa Johnson ambaye alilazwa baada ya hali yake kubadilika ghafla anaendelea vizuri hivi sasa.
Boris alilazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi kwa siku mbili baada ya hali yake kuzorota alipofikishwa hospital.
Wiki iliyopita, aligunduliwa kuwa na dalili za wastani za ugonjwa huo na kujitenga nyumabani kwake huku akiendelea kuongoza shughuli za serikali.
Lakini hali yake ikabadilika wiki hii na kulazimisha kupelekwa hospitali ambako bado anaendelea na matibabu.
Social Plugin