Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson ametoka hospitali baada ya kupona virusi vya corona lakini atapumzika kwanza kabla ya kuanza kurejelelea majukumu yake.
Johnson, 55, alipelekwa St Thomas' hospital, mjini London, Jumapili - siku ya 10 baada ya kupatatikana na virusi hivyo.
Alikuwa katika chumba cha wagonjwa mahututi kwa siku tatu kabla ya kurejeshwa kwenye wodi ya kawaida Alhamisi.
Kulingana na taarifa iliyotolewa, Waziri Mkuu ataendelea kupumzika katika makazi ya Chequers.
Idadi ya watu waliokufa kwa virusi vya corona nchini Uingereza inasemekana kupita 10,000 hadi kufikia Jumapili.