Watu 16 zaidi wameambukizwa corona nchini Kenya na kufanya idadi ya wagonjwa nchini Kenya kufikia 336.
Katibu wa Kudumu katika Wizara ya Afya Dkt Rashid Aman amewaambia waandishi wa habari leo Ijumaa, Aprili 24 kwamba wagonjwa hao walithibitishwa baada ya sampuli 946 kupimwa katika saa 24 zilizopita.
Amesema Visa 11 vimetokea Nairobi huku wagonjwa wengine 5 wakiwa Mombasa.
COVID-19 UPDATE✔️946 samples tested in the past 24 hours✔️16738 total samples tested✔️16 new positive cases today✔️Total confirmed cases stand at 336✔️Fatalities remain at 14✔️887 still being monitored#KomeshaCorona— Ministry of Health (@MOH_Kenya) April 24, 2020
Social Plugin