WATAALAMU WA SEKTA YA RASILIMALI WATU NA WADAU WA SEKTA YA UCHUMI KUKUTANA MTANDAONI

Wakati janga la Corona limeathiri njia za ufanyaji kazi duniani kote, kampuni nyingi duniani zimelazimika kutafuta namna mpya ya ufanyaji kazi.


 Nchini Tanzania, kampuni ya BrighterMonday Tanzania imeandaa semina ya mtandaoni itakayowakutanisha wataalamu katika sekta ya Rasilimali Watu pamoja na wadau katika sekta ya biashara kujadili mchango wa Rasilimali Watu katika kuhakikisha Uendelevu wa Biashara wakati wa mlipuko wa virusi Corona.  

Semina hiyo itafanyika Jumanne, Mei 12, 2020 kwa njia ya mtandao na kuwakutanisha waajiri na wadau mbalimbali wa uchumi na biashara kutoka nchini na nje ya Tanzania. Semina hiyo itaendeshwa na wabobevu katika sekta ya Rasilimali Watu, Bw. Mosses Raymond pamoja na Heather O'shea. Kwa mujibu wa mtandao wa BrighterMonday Tanzania, Maafisa Rasilimali Watu kote nchini wanakaribishwa kushiriki kwa kujisajili kupitia tovuti (https://bit.ly/2SLiDKb)   

Kupitia semina hiyo, wadau wa sekta ya uchumi hasa waajiri watanufaika na uzoefu kutoka kwa makampuni makubwa ambayo yatatoa uzoefu na mbinu za kuendelea na utendaji hasa wakati huu ambapo biashara zimekuwa katika mkwamo, washiriki watanufaika na mbinu za namna ya kuendelea kupata wataalamu, mbinu za namna kukabiliana na mabadiliko ya usaili na kupata wasaa wa kubadilishana mitazamo ya kitaalamu na manguli katika sekta ya rasilimali watu.  

BrighterMonday Tanzania wameandaa mfululizo wa semina kwa njia ya mtandao kama sehemu ya utekelezaji wa  programu yao inayokwenda kwa jina la 'Umoja Wakati wa Shida' yenye lengo la kuhakikisha uendelevu wa biashara wakati huu wa mlipuko wa virusi vya Corona. 

Je, ungependa kuwa sehemu ya semina hiyo ya mtadaoni? Tembelea tovuti hii https://bit.ly/2SLiDKb BOFYA HAPA

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post