Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) ametoa msaada wa Kompyuta mbili zenye thamani ya shilingi milioni 4 kwa ajili ya matumizi ya ofisi ya walimu wa Shule ya Sekondari Bulige na Ngaya zilizopo katika Halmashauri ya wilaya ya Msalala.
Akikabidhi Kompyuta hizo kwa Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha leo Jumamosi Mei 9, Mhe. Azza amesema Kompyuta hizo zitawasaidia walimu wa shule hizo katika shughuli zao.
“Nilitembelea shule ya Ngaya walimu wakaniomba niwachangie Computer. Leo nakabidhi Computer mbili zenye thamani ya shilingi 2,000,000 kila moja kwa ajili ya shule ya sekondari Bulige na Ngaya”,amesema Azza.
Kwa upande wake,Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha amemshukuru Mbunge Azza kwa kuchangia katika sekta ya elimu na kuongeza kuwa Kompyuta hizo zitasaidia kurahisha kazi za walimu na mawasiliano kwa njia ya mtandao wa Intaneti.
Kulia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha Kompyuta mbili zenye thamani ya shilingi milioni 4 kwa ajili ya matumizi ya ofisi ya walimu wa Shule ya Sekondari Bulige na Ngaya zilizopo katika Halmashauri ya wilaya ya Msalala. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kulia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha Kompyuta mbili zenye thamani ya shilingi milioni 4 kwa ajili ya matumizi ya ofisi ya walimu wa Shule ya Sekondari Bulige na Ngaya zilizopo katika Halmashauri ya wilaya ya Msalala.