Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) ametoa msaada wa Baiskeli Maalumu kwa kijana Fikiri Francis (17),mkazi wa kata ya Lunguya halmashauri ya wilaya ya Msalala wilayni Kahama aliyepata ulemavu baada ya kuanguka kwenye mti wa mwembe.
Mhe. Azza amemkabidhi baiskeli hiyo kijana Fikiri Francis leo Jumamosi Mei 9,2020 mbele ya Mkuu wa wilaya ya Kahama,Mhe. Anamringi Macha.
“Nilipewa taarifa na Diwani wa kata ya Lunguya mhe. Benedicto Manwali kuhusu kijana huyu ambaye alipata ajali na kuvunjika mgongo mwaka 2018 akapata ulemavu na hawezi kutembea.Nimetafuta baiskeli kwa ajili ya kijana huyu na leo namkabidhi ili imsaidie kusafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine”,amesema Azza.
Naye Kijana Fikiri Francis na Diwani wa kata ya Lunguya mhe. Benedicto Manwali wamemshukuru Mbunge huyo kwa msaada huo ambapo sasa hatatumia magongo ya mti kutembea.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha amemshukuru Mhe. Azza kwa kumsaidia baiskeli kijana huyo huku akimuomba kuendelea kusaidia watu wenye uhitaji katika jamii.
Wa pili kushoto ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akizungumza wakati akitoa msaada wa Baiskeli Maalumu kwa kijana Fikiri Francis (17),mkazi wa kata ya Lunguya halmashauri ya wilaya ya Msalala wilayani Kahama aliyepata ulemavu baada ya kuanguka kwenye mti wa mwembe. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha ( wa pili kushoto) akimshukuru Mbunge Azza kwa kumsaidia baiskeli kijana Fikiri Francis (aliyekaa kwenye kiti kilichotolewa na Mbunge Azza Hilal).
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha akimpa pole kijana Fikiri Francis kwa ajali iliyompata na kumsababishia ulemavu.