Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Dan Kazungu amesema kuwa, Rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta, anao upendo wa dhati kwa Watanzania kwani siku zote hutamani Wakenya na Watanzania kuwa kitu kimoja na ndiyo maana alikuwa Rais wa kwanza kwenda Chato kumsalimia Rais Magufuli.
Balozi Kazungu ameyabainisha hayo leo Mei 19, 2020, wakati akizungumza na waandishi wa habari na kuwaomba Watanzania kuwa na subra na kwamba ugonjwa wa Corona usiwe chanzo cha kuwagombanisha na badala yake wawaachie viongozi waweze kusuluhisha suala hilo.
“Rais Kenyatta amenituma hapa, anasema Kenya haiiangalii Tanzania kama jirani bali kama Ndugu, sisi sio maadui, adui yetu ni corona, ndio maana alikuwa Rais wa kwanza kuingia Chato kumsalimia Rais Magufuli, akachukua dhahabu akasema mpelekeeni Magufuli.
“Bila hii corona April 26 mwaka huu Kenyatta alipanga aje asherehekee na Watanzania Muungano, alipanga awe na ziara ya muda mrefu hapa TZ kuliko Rais yeyote, uamuzi ambao Kenya imechukua kuhusu safari za mipakani sio kwasababu ya Tanzania bali adui yetu ni kirusi
“Hakuna Mkenya anayemuombea mabaya Mtanzania, Wakenya tunawaombea Watanzania mpigane na janga hili, na sisi pia mtuombee, tusianze kukorogwa na kirusi hiki, tusianze kugongana kisa corona, Watu watulie, Viongozi wetu watakutana na tutalimaliza"-Amesema
Social Plugin