Mbunge wa Ndanda kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Cecil Mwambe, amesema kuwa kwa sasa amerejea Bungeni rasmi kumalizia muda wake wa Ubunge kwa kipindi kilichobaki na kwamba yeye ni mwanachama halali wa CCM, hivyo uchaguzi ujao atagombea kupitia tiketi ya CCM.
Mwambe ameyabainisha hayo leo Mei, 8, 2020, wakati akizungumza na Kituo cha EATV na kuongeza kuwa yeye ni kiongozi mtiifu hivyo aliona ni vyema kuitikia wito wa Spika Ndugai, na kwamba leo atakaa bungeni upande wa Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni Wilfred Lwakatare kwa kuwa ndiye anayemtambua kwa sasa.
"Nimefika Dodoma kama ambavyo nilisema, nimekutana na Mh Spika hivyo ninatakiwa kuendelea na shughuli zangu za Kibunge, mimi nitaendelea kuwa Mbunge wa CHADEMA na mchana huu nitahudhuria vikao vya Bunge, nilijiuzulu uanachama na nikaacha kila kitu hivyo Mh Spika amenitaka nimalizie kipindi kilichosalia" amesema Mbunge Mwambe.
Akizungumzia suala la kulipwa mishahara na posho zingine ilihali yeye si Mbunge, Mwambe amesema kuwa, "Mimi nasema kwamba Spika alikuwa halipi mshahara kwa Mbunge hewa, mimi nimelipwa mshahara wangu wa mwisho ni wa Februari 15, ambao nililipwa Machi na nilipewa nusu sababu ndiyo nilioufanyia kazi".
Social Plugin