Picha : WORLD VISION TANZANIA YATOA MSAADA WA VIFAA TIBA NA KINGA CORONA KWA WATOA HUDUMA ZA AFYA SHINYANGA

Shirika la World Vision Tanzania limetoa msaada wa vifaa tiba na kinga vyenye thamani ya shilingi milioni 29 kwa ajili ya kusaidia watumishi wa sekta ya afya katika mkoa wa Shinyanga kujikinga na Maambukizi ya Virusi vya Corona ‘Covid 19’ wanapohudumia wagonjwa.

Vifaa hivyo vimekabidhiwa leo Ijumaa Mei 8, 2020 na Meneja wa World Vision Tanzania Kanda ya Ziwa John Massenza kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga.

Massenza alisema wao kama wadau wa sekta ya afya wanaofanya kazi zao katika wilaya ya Shinyanga,Kahama na Kishapu jukumu lao kubwa sasa ni kushirikiana na serikali kupambana na janga la COVID -19 kwa kusaidia kuimarisha au kuboresha mifumo ya afya.

“Shirika la World Vision Tanzania Kanda ya Ziwa tumeleta vifaa vya kujikinga na COVID – 19 ambavyo vimenunuliwa kutoka MSD lakini Magauni yamenunuliwa kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya kusaidia watumishi wa sekta ya afya katika mkoa mzima wa Shinyanga”,alisema Massenza.

Alivitaja vifaa hivyo kuwa Vipaza sauti 243 ‘Megaphones’ kwa ajili ya watoa huduma ngazi ya jamii kutoa elimu ya Corona vijijini, Barakoa ‘ Surgical masks’ pea 1000, Vitakasa mikono ‘ Sanitizers’ lita 300, Magauni maalumu ya kujikinga‘ Personal Protective Equipments – PPE Gouwns’ 60, Gloves boksi 1000 vyote vikiwa na thamani ya shilingi 29,013,000/=.

Alisema mbali na kuchangia vifaa tiba na vifaa kinga, pia wametoa mafunzo kuhusu ugonjwa wa Corona kwa watoa huduma ngazi ya jamii 117,watoa huduma 132 kwenye vituo vya afya na madiwani 47 wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

“Kwa ujumla mchango wetu World Vision Tanzania katika mkoa wa Shinyanga mpaka sasa umegharimu shilingi 100,083,500/=,na tutaendelea kutoa mchango mpaka tutakapofanikiwa kumaliza tatizo hili la COVID 19”,alisema.

“Tunaishukuru serikali kwa ushirikiano inaotupatia katika mapambano dhidi ya COVID -19”,aliongeza Massenza.

Akipokea vifaa hivyo Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack alilishukuru Shirika la World Vision kwa mchango huo wa vifaa tiba akibainisha kuwa vitawasaidia watoa huduma za afya kuwa na amani wakati wa kwenda kuhudumia wagonjwa kwa sababu watakuwa na uhakika kuwa na wao wamejikinga dhidi ya maambukizi ya COVID – 19.

“Mimi niwashukuru sana World Vision, tuko pamoja na tutaendelea kushirikiana na naomba muendelee msichoke kutoa mchango kwa sababu ugonjwa huu siyo wa mtu hakuna anayenyoshewa kidole kuwa huyu atapata. Tunakijikinga sote, tunajikinga sisi ili pia tusiambukize na wengine lakini na wale tunaowakinga wakiweza kujikinga na sisi hatuwezi kuambukizwa",alisema Mhe. Telack. 

Mkuu huyo wa mkoa alitumia fursa hiyo kuwashukuru wadau wote wanaoendelea kushirikiana na serikali kukabiliana na ugonjwa wa Corona.

Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile alisema mchango huo wa vifaa utaongeza ari,nguvu na moyo kwa watumishi wa afya kuhakikisha kuwa wanatoa huduma stahiki kwa wagonjwa bila kusita,bila hofu wala mashaka.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Kushoto ni Meneja wa World Vision Tanzania Kanda ya Ziwa John Massenza akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack  gauni maalumu la kujikinga na maambukizi ya COVID -19' PPE Gouwns' ambalo ni sehemu ya magauni 60 yaliyolewa kwa ajili ya kusaidia watumishi wa sekta ya afya katika mkoa wa Shinyanga kujikinga na Maambukizi ya Virusi vya Corona ‘Covid 19’ wanapohudumia wagonjwa leo Ijumaa Mei 8,2020 katika Hospitali ya Rufaa mkoa wa Shinyanga. Kulia ni Mganga Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack  akiangalia gauni maalumu la kujikinga na maambukizi ya COVID -19' PPE Gouwns' ambalo ni sehemu ya magauni 60 yaliyolewa na Shirika la World Vision Tanzania kwa ajili ya kusaidia watumishi wa sekta ya afya katika mkoa wa Shinyanga kujikinga na Maambukizi ya Virusi vya Corona ‘Covid 19’ wanapohudumia wagonjwa.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack  akikagua gauni maalumu la kujikinga na maambukizi ya COVID -19' PPE Gouwns' ambalo ni sehemu ya magauni 60 yaliyolewa na Shirika la World Vision Tanzania kwa ajili ya kusaidia watumishi wa sekta ya afya katika mkoa wa Shinyanga kujikinga na Maambukizi ya Virusi vya Corona ‘Covid 19’ wanapohudumia wagonjwa.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akikagua vazi maalumu la kujikinga na maambukizi ya COVID -19' ambalo ni sehemu ya magauni 60 yaliyolewa na Shirika la World Vision Tanzania kwa ajili ya kusaidia watumishi wa sekta ya afya katika mkoa wa Shinyanga kujikinga na Maambukizi ya Virusi vya Corona ‘Covid 19’ wanapohudumia wagonjwa.
Kushoto ni Meneja wa World Vision Tanzania Kanda ya Ziwa John Massenza akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack Kipaza sauti na Gloves.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akiangalia moja Sanitizer ambayo ni sehemu ya lita 200 zilizotolewa na Shirika la World Vision Tanzania kwa ajili ya kusaidia watumishi wa sekta ya afya katika mkoa wa Shinyanga kujikinga na Maambukizi ya Virusi vya Corona ‘Covid 19’ wanapohudumia wagonjwa.
 Kulia ni Meneja wa World Vision Tanzania Kanda ya Ziwa John Massenza akizungumza wakati wa kukabidhi msaada wa vifaa tiba na kinga vyenye thamani ya shilingi milioni 29 kwa ajili ya kusaidia watumishi wa sekta ya afya katika mkoa wa Shinyanga kujikinga na Maambukizi ya Virusi vya Corona ‘Covid 19’ wanapohudumia wagonjwa.
Meneja wa World Vision Tanzania Kanda ya Ziwa John Massenza akielezea namna wanavyoshirikiana na serikali katika mapambano dhidi ya Virusi vya Corona.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akilishukuru Shirika la World Vision kwa mchango wa vifaa tiba na kueleza kuwa vitawasaidia watoa huduma za afya kuwa na amani wakati wa kwenda kuhudumia wagonjwa kwa sababu watakuwa na uhakika kuwa na wao wamejikinga dhidi ya maambukizi ya COVID – 19.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akiwashukuru wadau wanaoshirikiana na serikali katika mapambano dhidi ya Virusi vya Corona.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akiwasisitiza watumishi wa afya na wananchi kuendelea kuchukua tahadhari kuhusu ugonjwa wa Corona.
Watumishi wa afya katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga wakifuatilia zoezi la kukabidhi vifaa tiba na kinga vilivyotolewa na Shirika la World Vision Tanzania.
Mganga Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile akilishukuru Shirika la World Vision Tanzania kwa mchango wa vifaa tiba na kinga ambapo alisema mchango huo wa vifaa utaongeza ari,nguvu na moyo kwa watumishi wa afya kuhakikisha kuwa wanatoa huduma stahiki kwa wagonjwa bila kusita,bila hofu wala mashaka.
 Sehemu ya vifaa tiba na kinga vyenye thamani ya shilingi milioni 29 vilivyotolewa na Shirika la World Vision Tanzania limetoa kwa ajili ya kusaidia watumishi wa sekta ya afya katika mkoa wa Shinyanga kujikinga na Maambukizi ya Virusi vya Corona ‘Covid 19’ wanapohudumia wagonjwa.
 Sehemu ya vifaa tiba na kinga vyenye thamani ya shilingi milioni 29 vilivyotolewa na Shirika la World Vision Tanzania limetoa kwa ajili ya kusaidia watumishi wa sekta ya afya katika mkoa wa Shinyanga kujikinga na Maambukizi ya Virusi vya Corona ‘Covid 19’ wanapohudumia wagonjwa.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post