Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

CORONA YAFUTA TOFAUTI YA DAIMOND NA CLOUDS MEDIA ......KUSAGA AAGIZA NYIMBO YAKE IPIGWE REDIONI

CEO wa Clouds Media Group Joseph Kusaga amezindua kampeni ya BONGE LA MPAMBANAJI ambayo ni maalum kwa ajili ya kuwawezesha Wahudumu wa Afya Tanzania kwa vifaa tiba na mahitaji mengine kwenye vita hii dhidi ya kirusi cha corona.


Wakati akihojiwa na Power Breakfast ya Clouds FM Kusaga akasema anao Wapambanaji wenzake ambao wako tayari kuungana na yeye na miongoni mwao ni Vodacom, Tigo na Diamond Platnumz ambaye alimpigia simu LIVE na kuzungumza kwenye Power Breakfast.

Akiongea kwenye PB Diamond amesema “Kwanza nimpongeze CEO Kusaga kwa kuweka nguvu zake kwenye hilo sio kila Mtu mwenye moyo huo, mimi pia nitaweka mchango wangu hapo na kama unavyofahamu tayari pia upande wangu nimeanza kulipia kodi familia zilizokwama kutokana na hii corona”

Baada ya kuzungumzia Bonge la Mpambanaji, CEO Kusaga alimtaka Diamond achague wimbo wake ili uchezwe kwenye PB kuwaamsha Wapambanaji wote ambapo mara ya kwanza alipendekeza apigwe Msanii wake mpya @officialzuchu lakini baada ya Jo kusisitiza kuwa ngoma ya Diamond ndiyo inatakiwa, Platnumz alichagua yope remix na ikapigwa.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com