Mmiliki wa Kampuni ya SSMC Limited Saidi Mohamed kushoto akimkabidhi
vyakula vya futari na vifaa vya kujikinga na Ugonjwa wa Corona Diwani wa
Kata ya Makorora Omari Mzee vyenye thamani ya milioni 16 vilivyotolewa
na Kampuni ya Mafuta ya GP mapema leo kushoto ni Afisa Mtendaji wa Kata
ya Makorora Ramadhani Badi
Diwani
wa Kata ya Makorora Omari Mzee kushoto akibidhi mmoja wa wananchi wa
Kata ya Makorora Futari yenye thamani ya milioni 16 vilivyotolewa na
Kampuni ya Mafuta ya GP mapema leo ikiwemo vifaa vya kujikinga na Virusi
vya Corona
Diwani wa Kata ya Makorora Omari Mzee kulia akikabidhiwa vitakasa mikono (Sanitize ) na vyakula kutoka kwa Mmiliki wa Kampuni ya SSMC Limited Saidi Mohamed vyenye thamani ya milioni 16 vilivyotolewa na Kampuni ya Mafuta ya GP mapema leo
Diwani wa Kata ya Makorora Omari Mzee kulia akigawa msaada huo kwa wananchi wa mitaa mbalimbali kwenye Kata hiyo kulia ni Mmiliki wa Kampuni ya SSMC Limited Saidi Mohamed
Mmiliki wa Kampuni ya SSMC Limited Saidi Mohamed akiwaaonyesha waandishi wa habari vitakasa mikono ambavyo vimetolewa
DIWANI
wa Kata ya Makorora Jijini Tanga (CCM) Omari Mzee ameishukuru Kampuni
ya Mafuta ya GP kwa kutoa msaada futari kwa kaya 150 kwenye
kata yake ikiwemo vifaa vya kujikinga na ugonjwa wa Virusi vya Corona.
Huku
akiwataka wazazi na walezi kuhakikisha wanakuwa mstari wa mbele
kuwaelimisha watoto wao ili kuona ile mikusanyiko isiyokuwa ya lazima
waweze kuepukana nayo ikiwa ni mkakati wa kukabiliana na Ugonjwa wa
Virusi vya Corona ambayo kwa sasa vinaitikisha dunia.
Omari
aliyasema hayo leo wakati akipokea msaada huo wenye thamani ya Milioni 16 vilivyotolewa na
kampuni ya Mafuta ya GP vilikabidhiwa na Mmiliki wa Kampuni ya SSMC
Limited Saidi Mohamed kufuatia ombi la kumtaka ashirikiana nao kwenye
kukabidhi vyakula na vifaa hivyo..
Alisema vifaa hivyo vitawasaidia
wakati huu wa mwezi wa ramadhani ikiwemo katika kukabiliana dhidi ya
Ugonjwa huo wa Corona huku akiwataka wananchi kuendelea kuchukua
tahadhari ambazo zimekuwa zikitolewa na wataalamu wa Afya hapa nchini.
Aidha
alisema kwa sasa shule zimefungwa na watoto wamekuwa wakizagaa mitaani
hivyo wanapaswa kuchukua tahahdari kwa kuwaelimisha ili kuona ile
mikusunyiko ilisyokuwa ya lazima waweze kuepukana nayo kwa lengo la
kuwaepusha na maambukizi ambayo wanaweza kukumbana nayo.
“Nishukuru
sana kwa furari hii kwa zile kaya ambazo hawajiwezi zitawasaidia
kupunguzia makali ya maisha lakini wazazi tutambue ugonjwa huu wa Virusi
vya Corona upo hivyo niwasihi wazazi na jamii nzima kwa ujumla tuweza
kuchukua tahadhari kukabiliana nao “Alisema Diwani huyo.
Awali
akizungumza kabla ya makabidhiano hayo Mkurugenzi wa Kampuni ya SSMC
Limited Saidi Mohamed alisema kwamba wamekabidhi vyakula hivyo kwenye
kaya masikini 150 ambavyo vimetolewa na kampuni.
Ambapo
alisema kutokana na ukongwe wangu wa kampuni za Oili Mkoa wa Tanga
wamemuomba washirkiane nami kukabidhi vyakula hivyo kwa waliofunga mwezi
mtufuku na vifaa vya kujikinga dhidi ya Corona vyenye thamani ya
milioni 16.
Vifaa hivyo alivikabidhi kwa diwani wa Kata hiyo
Omari Mzee ili aweze kuvikabidhi kwa wananchi kwenye mitaa ili kuweza
kuwapunguzia makali ya maisha waliokuwa nao baadhi ya jamii maeneo hayo
kutokana na kushindwa ukata ambao wamekuwa wakikumbana nao.
Social Plugin