Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Jeshi la polisi mkoa wa Dodoma limekamata magari 17 yadhaniwayo kuwa ya wizi katika msako wa siku nne uliofanyika kati ya tarehe 19.5.2020 hadi tarehe 22.5 2020.
Hayo yamesemwa Mei 26,2020 na kamanda wa polisi Mkoa wa Dodoma Gilles Muroto wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema kuwa walimkamata Helman Stephen akiwa na gari namba T.891 BXY Toyota PREMIO gari ambalo linatumia kadi na usajili wa kubatizwa za gari lingine huku akisema kuwa walimkamata Athuman Juma Pambagu mwenye umri wa miaka 29 mkazi wa Nzuguni mwenye gari namba T.864 CQA TOYOTA IST chassis imekatwa na kuungwa kibati kiingine vioo vimefutwa na kubandikwa namba nyingine ambalo limebatizwa namba na card ya gari nyingine.
Aidha amesema kuwa wamekamata gari lenye namba ya T.237 DSJ aina ya SUBARU ni gari la transit {IT} lilikuwa linasafirishwa kwenda Uganda ambalo dereva alipakia abiria wawili huko MISUGUSUGU Pwani kwenda Kahama Shinyanga ambapo dereva alitishiwa silaha na kuporwa gari na kufungwa kamba na kutupwa porini eneo la Pandambili kongwa .
Sanajari na hayo Kamanda Muroto amesema kuwa walimkamata Festo Castory Lalika akiwa na vifaa vya pikipiki 4, jenereta mbili na engine moja ya bajaji huku pia akikamatwa Lello Michael Ringo akiwa na Tv 3 aina ya SAMSUNG,SUBWOFER 1 Vichwa vya cherehani 2,laptop 1 HP Stabilizer 2 ambazo ni mali za wizi na vifaa vya kuvunjia drill 1 na panga .
Hivyo amesisitiza watu waache kujihusisha na uhalifu wa aina yoyote ikiwa ni pamoja na wizi , na magari ya wizi wayasalimishe haraka katika kituo cha polisi kabla ya kukamatwa huku akiwashauri watu ambao wananunua magari wahakikishe wanayakagua magari hayo kabla ya kununua ili wasiingie katika matatizo ya kumiliki chombo cha wizi.