Waziri wa Afya nchini Kenya Mutahi Kagwe almetangaza kwamba visa vya maambukizi ya corona nchini humo vimefika 535 baada ya watu 45 zaidi kupatikana na maradhi hayo.
Kwenye hotuba yake kwa vyombo vya habari leo Jumanne, Mei 5, Kagwe amesema hii ni idadi kubwa zaidi kuwahi kurekodiwa tangu kisa cha kwanza cha COVID-19 kuripotiwa Machi 13, 2020.
Kati ya visa hivyo 45, 30 ni wanaume na 15 ni wanawake. Mutahi amesema kwamba watu 29 ni wakaazi wa Nairobi, 11 kutoka Mombasa na watano kutoka Wajir.
Social Plugin