Maambukizi ya virusi vya Corona duniani yamepindukia milioni 3.5 leo Jumatatu, wakati idadi ya vifo vinavyosababishwa na janga hilo imeongezeka hadi zaidi ya 245,000, ingawa viwango vya maambukizi mapya na vifo vimepungua ikilinganishwa na mwezi uliopita, kulingana na ripoti ya shirika la habari la Reuters.
Visa vingi vilivyothibitishwa katika siku za hivi karibuni viliripotiwa katika ukanda wa Amerika ya Kaskazini na nchi za Ulaya, ingawa idadi ya kila siku ya maambukizi mapya inaongezeka katika ukanda wa Amerika ya Kusini, Afrika na Urusi.
Duniani kote, visa vipya 84,004 viligunduliwa ndani ya masaa 24 yaliyopita, shirika la habari la Reuters limebaini, huku likijikita katika takwimu rasmi zilizotolewa na kila, idadi ambayo inafanya jumla ya visa duniani kote kufikia zaidi ya milioni 3.5.
Vifo vinavyotokana na mlipuko wa Covid-19, ugonjwa unaosababisha matatizo ya kupumua vimefikia jumla ya 245,992.
-RFI
Social Plugin