MAFURIKO YAUA WATU 194 NCHINI KENYA


Mvua kubwa zilizonyesha nchini Kenya zimeua  watu 194, kwa mujibu wa maafisa wakinukuliwa na vyombo vya habari nchini humo. 


Kwa mujibu wa  gazeti la kila siku la Daily Nation, watu 194 wamefariki dunia kote nchini kutokana na mvua kubwa zinazonyesha na kusababisha mafuriko.

Mamlaka nchini Kenya imewataka watu wanaoishi katika maeneo yanayokumbwa na mafuriko, kama vile kando ya mito, kuondoka haraka maeneo hayo.

Gazeti la Daily Nation limemnukuu  Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Fred Matiangi akisema kwamba viongozi wako tayari kuwatoa  "kwa nguvu" watu walio katika hatari .

"Hatuna chaguo jingine. Tutahamisha watu kwa nguvu, hata ikiwa tutawasafirisha wenyewe kwa malori, tutafanya hivyo," afisa mmoja ameliambia Gazeti la kila siku la Standard Digital.

Kwa wale ambao hawajui wapi pa kwenda, mamlaka imetenga shule zilizofungwa kwa sababu ya marufuku ya watu kutotembea kutokana na janga la Corona. Shule hizi zitatumiwa kama hifadhi kwa muda kwa familia zilizohamishwa.

Mamlaka pia inasema serikali itatoa msaada wa chakula, maji na fedha kupitia simu kwa familia zilizohamishwa.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post