Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Tanzia : MCHUNGAJI PETER MITI MINGI AFARIKI DUNIA


Mchungaji Peter Mingi wa Kanisa la Ghala la Chakula (Warehouse Christian Centre-WCC) pia Mkurugenzi wa Voice of Hope Ministry (VHM) inayojihusisha na huduma ya injili vijijini amefariki dunia usiku huu Jumapili Mei 3,2020. 

Mchungaji Msaidizi wa kanisa hilo Samwel, amethibitisha. 

Baada ya kulitumikia kanisa la TAG kwa miaka mingi kama mchungaji msaidizi na baadaye kuanzisha huduma ya injili vijijini - VHM, baadaye Mwalimu na Mchungaji Peter Mitimingi alianzisha kanisa lijulikano kwa jina la Ghala la chakula au kwa Kiingereza Warehouse Christian Centre - WCC jijini Dar es salaam. 

Mchungaji Miti Mingi ambaye ni Mshauri wa Saikolojia wa BLCCC, alifahamika zaidi kwa mahubiri na mafundisho yake kuhusu mahusiano na maisha ya ndoa yaliyoenea zaidi kupitia Mitandao ya Kijamii.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com