MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA AVIKUMBUSHA VYAMA VYA SIASA KUKABIDHI RATIBA ZAKE MAPEMA


Msajili wa vyama vya siasa, Jaji Francis Mtungi, amevikumbusha vyama vya siasa kukabidhi ratiba zake za mchakato wa mambo mbalimbali wanapoelekea kwenye uchaguzi mkuu.

Amesema kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa vinapaswa kumshirikisha Msajili kwenye ratiba zao ndani ya vyama kuhusu mchakato wa uchaguzi.

Amesema hadi sasa hakuna mabadiliko ya Uchaguzi Mkuu na kwamba licha ya uwapo wa ugonjwa wa corona, shughuli zitaendelea kama kawaida, lakini kwa tahadhari kubwa.

“Tulishawaandikia  kwa mujibu wa sheria ya vyama vikifikia kwenye mchakato wa uchaguzi wakumbuke kutupatia ratiba zao

“Hatuvizii  ili wakosee bali tunawakumbusha mapema kuweka wazi ratiba zao ili nasi tushiriki…wakienda kinyume tumepewa nguvu kisheria kuweka pingamizi,” alibainisha.

Hivi karibuni, vyama vya CCM, Chadema na ACT Wazalendo, vilitangaza kuanza michakato ya ndani kuelekea uchaguzi mkuu ambao umebakisha miezi mitano

Majukumu ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ni kusajili chama cha siasa kinachokidhi vigezo vya usajili kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992, ikiwamo kufuta chama chenye usajili wa muda au kudumu ambacho kwa mujibu wa sheria kimepoteza sifa ya usajili.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post